Kosa Langu - Diamond Platnumz

Kosa Langu - Diamond Platnumz

Альбом
A Boy From Tandale
Год
2018
Язык
`スワヒリ語`
Длительность
257850

以下は曲の歌詞です Kosa Langu 、アーティスト - Diamond Platnumz 翻訳付き

歌詞 " Kosa Langu "

原文と翻訳

Kosa Langu

Diamond Platnumz

Ah!

Barua yako uliyotuma kwa Ricardo Momo nimeisoma

Ila nimechelewa kuijibu sababu moyoni imenchoma

Eeh!

Nliyo yategemea

Tofauti na nlicho kiona

Hata naandika hii barua

Huku roho yangu inansonona

Umesema nichane nguo

Pia funguo umeirudisha sawa

Simu niziweke kituo na sio chaguo

Nikome kabisa sawa

Umesema hata ile picha nzuri nliyo kukumbatia

Niichane sawa

Ila kinachoniumiza

Mbona moja umesahau

Kosa Langu Kosa Langu

Hujaniambia

Na kuniacha peke yangu

Ukanikimbia

Ila mbona kosa langu

Hujaniambia

Nami nikabiki peke yangu

Ukanikimbia

Aah!

Mbona ukanichimbia kaburi

Ningari bado mzima

Niife nizikwe vizuri

Nipotee kabisa kimya

Licha ya matendo mazuri

Kwa upendo na heshima

Moto ukachochea tanuri

Ukachoma wangu mtimaa

Natamani hata ningepata nafasi

Muda wakati Kukutazama

Unione hata japo sura

Unitazame macho yangu

Mwenzako wimbi limenipiga kasi

Langu jahazi limezama

Mnyonge mwana Sanura

Wee ndio ulikuwa furaha yangu

Tatizo hata nkilia wa kunifuta machozi sina

Sawa na gari lisio na gear

La kuiforce ipande mlima

Ndio maana siishi kulalama

Japo jibu moja tuu

Linaloniumiza

Mwenzio bado sijaelewa

Kosa Langu Kosa Langu (Kosa Langu)

Hujaniambia (Hujaniambia)

Na kuniacha peke yangu (Peke yangu)

Ukanikimbia (Ukaenda)

Ila mbona Kosa Langu (Kosa Langu)

Hujaniambia (Hujaniambia Bado)

Nami nikabi peke yangu (Peke yangu)

Ukanikimbia (Ukaenda Ooh!)

Oh moyo!

Moyo wangu umevunjika una magongo

Oh moyo!

Kila sehemu nayoshika kinyamazongo

Oh moyo!

Hata chozi likifutika linabaki tongo

Oh moyo!

Najitahidi kulidhika ila nna kinyongo

Oh moyo!

Moyo wangu umevunjika Unaa jamani

Oh moyo!

Hhhhmm hmm

200万曲以上の歌詞

様々な言語の楽曲

翻訳

あらゆる言語への高品質な翻訳

クイック検索

必要なテキストを数秒で見つけます