Amen - LADY JAYDEE

Amen - LADY JAYDEE

Год
2020
Язык
`スワヒリ語`
Длительность
204590

以下は曲の歌詞です Amen 、アーティスト - LADY JAYDEE 翻訳付き

歌詞 " Amen "

原文と翻訳

Amen

LADY JAYDEE

Uh hebu tazameni

Matendo ya Mungu yanavyotisha

Amefanya mengi makubwa ya kustaajabisha

Marafiki leo wana upendo kesho umekwisha

Ila upendo wa Mungu hauwezi kwisha

Naamini neno lako linaishi forever

Utendawazi hauwezi kubadili

Dhambi ikawa haki, Never!

Umenifikisha sehemu ambazo

Wala sikuwahi kuzifikiria

Sifa zako nitazihadithia

Unaniepusha na maadui

Unanilinda na mabaya

Ambayo hata siyatambui

Mungu uliye hai

Hata mimba zilizotokea

Kwenye mazingira ya dhambi

Watoto umewapa uhai

Na kama pumzi unanipa bure

Sasa kivipi tamaa ya pesa initenge na wewe

Nashukuru kwa kunileta hii sayari

Milele nitakuamini Mungu wa kweli AMINA

Amen Baba, Amen

Upendo wako, huruma yako Amen

Wema wako utukufu wako, Amen

Amen Baba, Amen

Umenipa maarifa, umenipa uhai, umenipa mali

Hata nacho kipaji siwezi sema sijaridhika

Umenipa kile ulichonipa, hukunitupa

Nami sitakijuta Baba, nasema AMEN

Glory to God, utajiri mkubwa ni furaha

Mungu anaweza kubariki mpaka ukashangaa

Niwapo kwenye njaa nikumbushe kwamba

Ndege hawalimi, hawavuni ila hawakosi chochote

Nilipotoka usiache nikumbusha

Nipe hekima nisitamani magari

Nisiyoweza kuyaendesha

Niishi kwenye ukweli nidumu

Maana uwongo hauishi milele

Na unaua faster kuliko sumu

Pia asante kwa kunipa bidii

Napokuomba haujibu haraka

Unajibu wakati sahihi

Una hekima inayoshangaza dunia

Watu hata tungombane vipi

Tunashare mvua na jua

Nilijalie nisilewe sifa

Nikumbuke siku za uhai wangu zinahesabika

Hivyo nikuabudu nikiwa kijana

Nawe utaniweka juu kwa baraka leo zaidi ya jana

Amen Baba, Amen

Upendo wako, huruma yako Amen

Wema wako utukufu wako, Amen

Amen Baba, Amen

Copyrights: Bongo Records Tanzania

このアーティストの他の曲:

200万曲以上の歌詞

様々な言語の楽曲

翻訳

あらゆる言語への高品質な翻訳

クイック検索

必要なテキストを数秒で見つけます